Later on Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ila alikanusha jina la Tunda Man kuwepo kwenye idadi ya walijeruhiwa kwenye ajali hiyo na kuthibitisha kuwa ajali hiyo ilisababisha kifo cha dereva wa gari lililopata ajali aliefahamika la Musa Katuzo maarufu kama Man Katuzo.
Marehemu,Man Katuzo.
Hata hivyo inaonekana kama Tunda Man alikua akitumia ajali hiyo kama “Kiki” kama watoto wa mjini wanavyosema kwani,kupitia akaunti yake Facebook,afisa uhusiano wa kituo cha redio cha Ebony Fm kituo ambacho Tunda Man na wenzake walifanya promo interview ya show zao,Luther Akyoo alikanusha Tunda Man kuwepo kwenye gari iliyopata ajali.
Taarifa za Uhakika kutoka kwenye chanzo chetu cha habari (jina kapuni)zinadai kuwa Man Katuzo ambae pia ni mwanamuziki,ndie aliekua promota wa show ambazo Tunda Man alifanya mkoani Iringa hali iliyopelekea familia ya marehemu kuchukizwa kwa kitendo cha Tunda Man kumuita marehemu dereva,wakati akijua wazi wasifu wa marehemu,Man Katunzo.
Tunda Man.
Kilichowasikitisha zaidi watu ni kitendo cha Tunda kuamua kurudi Dar es salam akitokea Iringa na kuuacha mwili wa marehemu na majeruhi hospitali huku akidaiwa kuondoka na camera mbili mali za marehemu ambapo mara baada ya tetesi za camera hizo kuchukuliwa na Tunda na wenzake kuvuja,jeshi la polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro walifanikisha kupekuliwa kwa gari alilokuwemo Tunda Man na wenzake eneo la Mikumi,Morogoro ambapo mara baada ya upekuzi walikutwa na camera hizo.Chanzo chetu cha habari kilienda mbali na kudai kuwa achilia mbali urafiki ambao Tunda Man na Man Katuzo walikua nao,Tunda Man hakufika kwenye msiba wa rafiki yake huyo kitendo kinachoonesha ni kwa kiasi gani Tunda Man alivyokosa ubinadamu.
Credit : Clouds Fm.
0 comments: