Jeshi
la Polisi Mkoani Arusha, limemkamata Isaack Habakuk Emily, kwa kosa la
kumtukana Rais John Magufuli kuwa ni bwege na kwamba hawezi fananishwa
na Nyerere na kusambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza
ofisini kwake, leo jijini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Charles Mkumbo, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 22 mwaka
huu eneo la Hotel ya Anex jijini humo.
Amesema
kuwa baada ya kumkamata alifanyiwa upekuzi na kukutwa na simu ya
kiganjani aina ya Tecno iliyotumika kutenda kosa la kutuma ujumbe wa
kumkashifu Dkt. Magufuli.
Mkumbo
amesema kuwa mtuhumiwa huyo alituma ujumbe wa kashfa kwenye Facebook
usemao:- “Mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere,” na kutuma kwa watu
mbalimbali kupitia simu yake ya mkononi.
Mkumbo
amesema mtuhumiwa baada ya kusikia hivyo aliandika tena ujumbe kwenye
mtandao wake usemao, “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu
bwege na Nyerere wapi Bwana,” amesema.
Amesema
baada ya kutuma ujumbe huo uliwaudhi watu wengi waliopokea ujumbe huo
na kuwakwaza, hali iliyosababisha kupeleka malalamiko yao Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka hiyo ilitoa taarifa
polisi na hatua za kisheria zilianza kuchukuliwa.
Aidha
amesema baada ya hapo walifanikiwa kumpata mtuhumiwa wa uhalifu kwa
njia ya mtandao, kumtia hatiani na jana alifikishwa mahakamani kujibu
shitaka lake.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi limetoa rai wa watu wote kutumia mitandao ya
kijamii vizuri kwa kujiletea maendeleo na kubadilishana taarifa zenye
tija na siyo zenye kuvunja sheria.
Pia amesema Jeshi hilo limejipanga kuwatia nguvuni wale wote watakaovunja sheria kwa kutumia mitandao ya kijamii.
0 comments: