Jeshi
la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Mganga wa Zahanati ya kijiji cha
Kidahwe wilayani Kigoma kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekuwa akimtibu
katika zahanati ya kijiji hicho.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Ferdinand Mtui amemtaja mganga huyo kuwa ni Ibrahim Bundala (29)na
kwamba anatuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 aliyefika
katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupata matibabu.
Amesema
mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi
kukamilika alitenda kosa hilo baada ya binti huyo kuingia katika chumba
cha daktari kwa ajili ya kumueleza ugonjwa anaoumwa.
Katika
tukio jingine wahamiaji 55 toka Burundi wamekamatwa katika maeneo
mbalimbali baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na wamekabidhiwa
idara ya uhamiaji kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na
kuwafikisha mahakamani.
0 comments: