Chelsea wanasubiria kumfanyia Diego Costa vipimo vya afya kabla ya
kumaliza uhamisho wa mshambuliaji huyo utakaogharimu pauni milioni 32
akitokea Atletico Madrid.
Uhamisho wa Costa Stamford Bridge, ambao ulikubaliwa kisheria wiki
iliyopita, ulifanyika huku mshambuliaji huyo akiuguza majeraha. Ila
Costa anarejea kufanya mazoezi na timu ya Hispania kuelekea Kombe la
Dunia huku Chelsea wakidhamiria kumaliza suala la matibabu.
Chelsea watamaliza uhamisho huo mwishoni mwa wiki hii na wanaamini utamalizika kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia wiki ijayo.
Kumleta Costa Chelsea mapema kwenye msimu huu wa jua (kiangazi)
kutamfanya Jose Mourinho aangalie wachezaji wengine, akiwemo Cesc
Fabregas, Ezequiel Lavezzi, Koke na Filipe Luis.
Kuja mapema kwa Costa kutaipa Chelsea nafasi ya kuanza kujaribu
kutafuta vilabu kwa washambuliaji wake Fernando Torres na Demba Ba.
Mustakabali wa Romelu Lukaku bado uko mashakani, akiwemo Samuel Eto’o
ambaye mkataba wake unakaribia kuisha.
0 comments: