Oparesheni 55 za vichwa vikubwa zafanikiwa Bugando
Jumla ya watoto 55 wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi, iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo, chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation. Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima.
Dk Kiloloma
Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma, ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.
Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.
Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii, jumla ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.
Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
“Watoto wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina”, alifafanua Dk Kiloloma.
Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi?
Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio wadhamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za GSM.
Kiwamba amesema taasisi yake ina lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa ya kesho wanao msingi wa nguvu kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu vikubwa ni elimu boira pamoja na Afya.
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM Shannon Kiwamba amesema wakati mwingine ni vigumu kuingia katika maisha ya kila mwananchi na kumsaidia mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika wa Afya na elimu anaweza kwenda mbali akijumlisha na jitihada zake.
Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo.
Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.
0 comments: