Al-Shabaab kwa mara nyingine tena imezidisha udhibiti wao juu ya watu wa Barawe kwa kunyang'anya vifaa vyote vya simu za mkononi zenya kamera, wakaazi waliiambia Sabahi.Kwa kutumia kipaza sauti hapo tarehe 10 Machi, wanamgambo wa al-Shabaab walitangaza azma mpya, kuwaagiza wakaazi wote kukabidhi simu zao za mkononi katika kambi ya al-Shabaab katika ofisi za manispaa ya Barawe, na kutishia adhabu kali kwa kutokutii amri hiyo."Watu ambao walikuwa wanachama wa al-Shabaab bila kutarajia walikuja dukani kwangu na kunilazimisha niwaonyeshe simu niliyokuwa ninatumia," alisema Farhan Mohamed, mwenye umri wa miaka 38, ambaye anamiliki duka la chakula katika soko Barawe. "Wakati nilipowaonyesha simu yangu, ambayo ilikuwa Nokia C3, waliichukua. Naweza kueleza tendo hilo kama ni sawa na wizi.""Walituambia kupitia vipaza sauti kwamba mtu yeyote ambaye anatumia simu yenye kamera na kushindwa kuiwasilisha kwao atakabliwa na adhabu kali," aliiambia Sabahi. "Watu wengi wameanza kupeleka simu zao zenye kamera, ziwe za aina yoyote, katika makao makuu ya al-Shabaab kutokana na hofu.""Dini ya Kiislamu haina vikwazo kwa kile ambacho al-Shabaab wanafanya, ambacho ni matumizi mabaya ya maisha ya watu na mali zao," Mohamed alisema.
Al-Shabaab 'lina hofu kubwa' ya majasusi
Hii si mara ya kwanza kwa al-Shabaab kuchukua hatua kali dhidi ya vyombo vya habari na mawasiliano ya simu katika maeneo yaliyo chini ya utawala wao.Mwezi Novembaa mwaka jana, kufuatia jaribio la kumkamata kiongozi mwandamizi wa al-Shabaab Abdulkadir Mohamed Abdulkadir (Ikrima)lililofanywa na jeshi la Marekani la Navy SEALs mwezi Oktoba, al-Shabaab iliwapiga marufuku watu wa Barawe wasiangalie televisheni, kwa kusema kwamba inaharibu misingi ya Kiislamu, na kuamrisha wakabidhi televisheni na satelaiti zao kwa maafisa wa al-Shabaab.Pia tangu ulipofanyika uvamizi huo, al-Shabaab ilianza kuwanyanyasa watu wanaotumia smartphones, kwa kusema kuwa vifaa vya simu vya teknolojia ya hali ya juu vinaweza kutumika kwa kufanyia upelelezi.Mzee wa Barawe Warsame Ali, mwenye umri wa miaka 49, alisema al-Shabaab ilikuwa inachukua hatua hizi kutokana na shinikizo kubwa na hofu wwaliyonayo baada ya wanajeshi wa Jeshi la Taifa la Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kuanzisha mashambulizi yao ya kijeshi."Al-Shabaab ni waoga sana," Ali aliiambia Sabahi. "Wakati askari wa AMISOM hivi karibuni walipoanza kuwafukuza kutoka miji mingi na kugundua kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi, walianza namna ya kuadhibu na kuwanyanyasa zaidi wakazi wa Barawe ili watu wasifahamu hasara wanazopata al-Shabaab na [ili kuhakikisha] kwamba mtu yeyote ambaye anayewapeleleza hawataweza kuishi huko."Ali alisema alikuwa na kamera kwenye simu yake ya mkononi, lakini hata kama haiwezi kuchukua picha, al-Shabaab ilimnyang'anya hata hivyo."Jambo la kushangaza ni kwamba simu yangu ilichukuliwa kwa nguvu wakati nilipokuwa ninawaambia kwamba kamera ilikuwa haifanyi kazi na hata hawakuiangalia," alisema. "Watu hawa hawakuwa hata na maarifa yoyote kuhusu simu zipi zinazo kamera zinazofanya kazi na zipi hazifanyi kazi. Mawazo yao yamekwama kwenye amri waliopewa."Ali alitoa wito kwa majeshi ya washirika kuja haraka kuwaokoa raia wa wilaya ya Barawe."Kwa unyenyekevu ninawaomba askari wa AMISOM na wale wa Jeshi letu la Taifa la Somalia kuukomboa mji huu kama amabvyo waliikomboa miji mengine ambako al-Shabaab walifukuzwa," alisema. "Ndoto yetu iliyo bora kabisa ni kuona Barawe inakombolewa kutoka kwa al-Shabaab. Sisi ni watu tunaofanyiwa vitendo vya kinyama ambao hatuwezi kujikomboa wenyewe kutokana na dhulma tunayofanyiwa na wao."
Bei zaongezeka maradufu kwa simu za mkononi zisizo kamera
Mkaazi wa Barawe Asha Mudey mwenye umri wa miaka 38 na mama wa watoot sita, aliiambia Sabahi kwamba wanachama wa al-Shabaab walikwenda nyumbani kwake alasiri moja na kuchukua simu yenye thamani ya dola 900 kutoka kwa jamaa zake sita ambao wanaishi nyumbani kwake."Tuliingiwa na hofu wakati wanachama wa al-Shabaab walipoingia ndani ya nyumba zetu na kuchukua simu za kila mtu," alisema. "Nililazimishwa hata kumuamsha mume wangu ambaye alikuwa amelala ili waweze kujua kama simu yake ilikuwa simu yenye kamera.""Ni mama yangu tu, ambaye alikuwa na simu ambayo haina kamera, aliyeachiwa simu yake," Mudey alisema."Pamoja na kwamba hali ya maisha yetu ilikuwa sio nzuri, al-Shabaab walituongezea tatizo hilo kwa kutunyang'anya simu zetu," alisema, akiongeza kuwa walilazimika kutumia dola 360 kwa kununua simu mpya zisizo kamera.Bei ya simu za mkono bila kamera imepanda huko Barawe tangu agizo la al-Shabaab, kwa mujibu wa Salim Abdi, mwenye umri wa miaka 36, ambaye anamiliki duka la simu za mkononi katika mji huo."Siku hizi simu za mkononi bila kamera ambazo tunauza ni ghali kwa sababu mahitaji yameongezeka kutoka kwa watu ambao wanataka kuzitumia," aliiambia Sabahi. "Kwa mfano, tulikuwa tunauza Nokia 101, ambayo haina kamera, kwa dola 30 na sasa ni dola 60."Abdi alisema alikuwa anatekeleza maagizo al-Shabaab kwa kuhofia usalama wake, si kwa sababu ya faida yoyote kiuchumi."Tumezirejesha simu za kamera Mogadishu kwa sababu hakuna mtu wa kuzinunua hapa kwa vile kila mtu anaogopa al-Shabaab," alisema.
Je, unaipenda makala hii?
0 comments: