JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa kiwanda chakutengeneza Pombe "Feki" aina ya Konyagi huku likiwashikilia watu nanewaliokutwa ndani ya kiwanda hicho wakifanya shughuli ya utengenezajiwa pombe hiyo.Mbali na kiwanda na watuhumiwa hao pia Polisi imefanikiwa kunasamitambo mbalimbali iliyokuwa ikitumika kiwandani hapo zikiwemomalighafi zilizokuwa zikitumika kufunga bidhaa hizo kabla ya kuuzwakatika maduka ya jumla ya kuuzia Pombe.Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishana mwandamizi msaidizi wapolisi,Robert Boaz alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao Machi 14mwaka huu majira ya saa 7:00 Mchana katika eneo la Kambi ya raha njekidogo ya mji wa Bomang'ombe. "Askari polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hawa baada yawananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa utengezaji wa Pombe ambayohaijaruhusiwa kisheria ikiwa na nembo ya Konyagi ndipo askari walianzauchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watu hao katika nyumbainayomilikiwa na Elias Samson mwenye umri wa miaka 31"alisema Boaz.Kamanda Boaz alisema watuhummiwa hao pia walikutwa na lita 400 zapombe ikiwa imehifadhiwa katika mapipa tayari kwa ajili ya kujazwakatika vifungashio pamoja na Katoni 46 za pombe hiyo zote zikiwa nanembo ya Konyagi.Mbali na vitu hivyo Boaz pia alisema watu hao walikutwa na Makashatupu 178 ya kuhifadhi Konyagi yakiwa na nembo ,Pipa tupu 10zinazoaminika kuhifadhia pombe hiyo wakati wa utengenezaji na Mihurimiwili inayoonesha tarehe ya kutengezea na taraehe ya mwisho wamatumizi ya bidhaa ."Katika vitu vingine tulivyo wakuta navyo ni pamoja na majiko yamafuta "Ya Mchina"zaidi ya matano,vifaa vingine ambavyo ni kama Pasivilivyokuwa vikitumika kwa ajili ya kuchomea karatasi za nailoni baadaya kujaza hiyo Pombe"alisema Boaz.Kamanda Boaz aliyetembelea eneo kilipokuwepo kiwanda hicho aliwatajawaliokamatwa kuwa ni pamoja na George Kisivani (28), Yusuf George(33), Preygod Urassa (27) na Richard Leonard (35) Hagai Nelson (38),Jackson Shayo (29), Greyson Jonathan (27) wote wakazi wa Arusha pamojana Mohamed Rashidi (44) mkazi wa Dar es Salaam.Makasha na vifungashio vyakutwa na alama ya TBS na TRA.Katika hali isiyo ya kawaida Makasha ya bidhaa hiyo Feki yamekutwayakiwa na alama ya Ubora itolewayo na shirika la viwango Tanzania,(TBS) huku karatasi zenye Pombe zikiwa zimebandikwa karatasiinayotumiwa na mamlaka ya mapato nchini (TRA).Kamanda Boaz alisema uwepo wa alama hizo mbili ni kutaka kumuaminishamnunuzi pamoja na mtumiaji wa bidhaa hiyo kuwa ni halali naimethibitishwa na taasisi hizo mbili muhimu zinazosimamia Ubora wabidhaa pamoja na mapato.Alisema uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini watengezaji waMakasha hayo,pamoja upatikanaji wa alama hizo za TRA huku akiongezakuwa mbali na kosa hilo la kutengeneza bidhaa bandia pia watu haowanashiriki katika kuhujumu Uchumi wa nchi. "Huu ni uhujumu Uchumi kwa sababu wametengeneza bidhaa feki ,harafuwanaziuza madukani bila ya kulipia kodi,wakiwaaminisha wauzaji wenginena watumiaji kuwa bidhaa yao imethibitishwa na TBS na wanalipa kodikwa kuweka alama ya TRA"alisema Boaz.Kutokana na hali hiyo kamanda Boaz alisema tayari amefanya mawaslianona Uongozi wa shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka yamapato nchni (TRA) ili kuondoa utata uliopo hku akiongeza haja yakutolewa kwa elimu ili kuzuia athari za matumizi ya bidhaa zisizokuwana ubora
JESHI LA POLISI LANASA KIWANDA FEKI CHA KONYAGI
Previous Post
Tuzo ya mwalimu bora duniani yazinduliwa
Next Post
VIDEO, NGWAIR FT MIRROR ...ALAMA
0 comments: