Mwanamke wa miaka 20 amekunywa sumu mpaka kufa baada ya kufumaniwa na mumewe akifanya mapenzi na mjomba wa mume huyo jumapili iliyopita. Msemaji wa jeshi la polisi wa Mashonaland inspekta msaidizi Nobert Muzondo amekiri kutokea tukio hilo. Alimtambua marehemu kuwa ni Molyn Mudonhi wa mtaa wa 4232 barabara ya Sangano, Rusike Park. Inspekta anasema uchunguzi wa tukio hilo unaendela. Anasema siku ya tukio mnamo saa moja jioni, mume wa Mudonhi, Regway Matimaka alirudi nyumbani na kumkuta mke wake akifanya mapenzi na mjomba wake. Ugomvi ulizuka kati ya Matimaka na mjomba wake hali iliyosababisha Mudonhi kunywa sumu. Baada ya kugundua kuwa Mudonhi amekunywa sumu, Matimaka na mjomba wake walishirikiana kumkimbiza MKE WAO katika hospitali ya Marondera ambako alifariki dunia baada ya kuchekiwa na daktari. Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha maiti ili kufanya uchunguzi zaidi ya ki-daktari. Inspekta Muzondo alisema watu wanabidi watambue umuhimu wa maisha na mara zote watafute ushauri kutoka kwa wataalamu wa kisaikolojia.
Home
Local News
MKE ANYWA SUMU NA KUFA BAADA YA KUFUMANIWA NA MUME AKIFANYA MAPENZI NA MJOMBA WA MUMEWE
0 comments: