Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ni miongoni mwa wazee wa long time kwenye Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambapo time hii amepata nafasi ya kuwepo kwenye bunge la katiba linaloendela 104.4 Dodoma.March 20 2014 saa mbili kasoro usiku alisimama na kutumia zaidi ya dakika kumi kutoa yake ya moyoni kuhusu katiba na tofauti zilizopo kwenye katiba.1. Alianza kwa kusema ‘kwa ujumla nchi zetu zina hali moja kwamba bado ziko nyuma kiuchumi na ni tegemezi, wa Ulaya wako mbali sana kimaendeleo na ndio walitutawala…. wa Asia na wao walitawaliwa na haohao wa Magharibi lakini sisi tumebaki nyuma na tegemezi, wenzetu wa Asia wanaondokana na uchumi ulio nyuma na tegemezi kwa haraka sana’2. ‘Nilidhani katiba ni dira ya maendeleo ya watu wa nchi na nchi zote zina katiba, kwa nini sisi tuna katiba lakini maendeleo tatizo? hapa kwetu Mwalimu alituambia tulipopata Uhuru kwamba tukimbie wakati wenzetu wanatembea’3.‘Inaonekana tofauti kati ya sisi na wale waliotutawala inazidi kupanuka, tunachoita maendeleo ni vichekesho kwa sababu sisi ni watumiaji wa mambo ya maendeleo lakini sio waundaji wala sio watengenezaji kwa hiyo tunabaki nyuma’4. Katiba hizi za Afrika chache nilizoziona zinatilia mkazo mkubwa sana maswala ya mtandao wa madaraka, hata rasimu niliyoletewa juzi ni mfumo tu wa madaraka…5. Ukisoma mule na kwenye katiba iliyopita kuna maneno mazuri sanaaaa ya haki za binadamu lakini kwa sababu nchi yetu iko nyuma bado, wanaoweza kufaidi hayo yanayosemwa vizuri ya haki za binadamu ni kikundi cha watu wachache.6. Sisi tumepewa kazi ya kuunda katiba, nimepitia ile rasimu haizungumzii hatma ya makundi makubwa katika nchi yetu ambayo tumeyaweka pembeni tangu tupate uhuru, Wafugaji wahamaji, wavuvi, wakulima n.k …hali yao ilivyokua wakati wa mkoloni na sasa hivi tofauti yake ni ndogo sana.7. Hasa hawa Wafugaji wahamaji wanafukuzwa huku wanafukuzwa huko ndio hatma yao, katiba inatajataja tu habari za Wakulima, mara Wafugaji… ni kutaja tu, sasa nasema wenzetu wa Asia hizi katiba zao hazizungumzii habari za uchumi wao? kwa sababu kama uchumi wetu uko nyuma… swala la msingi ni kwamba katiba itoe maelekezo juu ya namna ya kutoka hapa kwenye uchumi ulio nyuma kwenda kwenye uchumi ulioendelea.8. Hivi haya mambo ya Makatiba tunaandika sisi haya ya kupiga maneno juu ya kugawana vyeo, hivi ndivyo wenzetu…..? manake kazi yetu sisi kuwasifu tu, Wachina wanakwenda, Wajapan wanakwenda…. hivi katiba zao wenzetu ndivyo wanavyoandika hivi?
0 comments: