Hai.
ZAIDI ya abiria 40 waliokuwa katika basi la Urio
linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Lushoto-Tanga wamejeruhiwa
vibaya baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepa basi jingine
katika makutano ya barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio walisema
ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni jirani kabisa na kituo cha mafuta
kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha wakati magari hayo yakijiandaa
kuanza safari mara baada ya kuzuiliwa kwa muda kupisha msafara wa Rais Kikwete.
Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo
lilipinduka wakati likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha
ambayo yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea
kwa ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea ikiwa ni muda mchache msafara wa
raisi Jakaya Kikwete kupita katika eneo hilo ukielekea uwanaja wa ndege wa KIA
, ukitokea wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambako Amefanya ziara ya siku
mbili.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema baada ya msafara wa
rais kupita magari yaliyokuwa yamesimamishwa kwa muda mrefu yaliondoka bila ya
kuwa na mpangilio maalum hali iliyosababisha kutokee kwa ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz
hakuweza kupataikana mara moja kuzungumzia ajali hiyo kutokana na ugeni wa rais
huku simu yake ikiita mara kadhaa bila ya kupokelewa .
Mwisho.
0 comments: