MARIAMU
HUSSEIN akiwa na hali mbaya baada ya kuchomwa kisu mgongoni na kwenye
paja wakati alipovamiwa na mwanamke mmoja ambaye inadaiwa kuwa Mariamu
alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa mwanamke huyo.Katika mkasa
huo ilielezwa kuwa Mariamu akiwa nyumbani kwao ghafla alifika mwanamke
huyo na kudai kuwa amekuja kutekeleza mauaji kwa kile kilichofahamika
kuwa amekuwa akivumilia kwa muda mrefu kuchukuliwa mume wake pasipo
kuleta fujo yeyote jambo ambalo lilionesha unyonge wa hali ya juu kwa
mwanamke huyo ambaye alifika nyumbani hapo na kucharuka kama Mbogo
aliyejeruhiwa na kuanza kufanya unyama huo. |
0 comments: