Tuesday, 29 April 2014

BILLIONAIRE MMOJA WA MADINI AACHIWA HURU KATIKA KESI YA MAUAJI YA ERASTO MSUYA

OFISI ya mkurugenzi wa Mashtaka Nchini imemfutia
mashtaka ya mauaji,mmoja kati ya watuhumiwa nane wa
mauaji ya kukusudia dhidi ya
mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite bilionea , Erasto
Msuya (43).
Hati ambayo imetumika kumwachia huru Joseph Damas
(Chusa) ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa madini
hayo imetolewa na kusainiwa na
mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Elieza Feleshi na
kisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuiwasilisha
kwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Munga Sabuni .
Hati hiyo ambayo hufahamika kama “Nolle Prosecution
“ilitolewa mbele ya mahakama hiyo April 16 mwaka huu
kwa ajili ya kuingiza rasmi katika kumbukumbu za
Mahakama.
“Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii, umekamilika
na ikikupendeza, upande wa mashitaka tunaomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya
mashahidi kabla ya kulipeleka jalada lenye mashitaka
haya, Mahakama Kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa
kesi ya mauaji ya kukusudia namba 06 ya mwaka
2013.”alieleza Julius Semali wakili wa serikali.
“Tumepokea hati ya kuachiwa huru kwa mshitakiwa namba
07, Joseph Damas,”alisema Wakili Semali.
Baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo, Hakimu Munga
aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 06 mwaka huu na kuamuru
washitakiwa saba, waliosalia katika kesi hiyo kurejea
rumande hadi hapo, shauri hilo litakapotajwa
tena mahakamani hapo ikiwa ni kwa ajili ya kusoma
maelezo ya mashahidi.
Bilionea Msuya aliuawa mwezi Agosti mwaka jana kwa
kupigwa, majira ya saa 6:30 mchana kando ya barabara
kuu ya Arusha-Moshi, eneo la Mijohoroni, Wilaya ya Hai,
Karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) na kufa papo hapo.
Washitakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji ya
kukusudia ni Sharif Mohamed Athuman (31), Mchimbaji
mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha,
Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredii (38), mkazi
wa Songambele Wilaya ya Simanjiro na Mussa Juma
Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu mkoani
Arusha.
Wengine ni Jalila Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki
Mohammed Jabir a.k.a “Msudani” au “Mnubi”(32), mkazi
wa Dar es salaam na Lang’ata Wilayani Hai, Karim
Kihundwa (33), mkazi wa Kijiji cha
Lawate, Wilaya ya Siha na Alli Musa Majeshi, mkazi wa
Babati mkoa wa Manyara.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: