Tuesday, 29 April 2014

Wasusia mechi kufuatia matamshi ya kibaguzi



Wachezaji wa timu ya Clippers
Shirikisho la mchezo wa vikapu nchini Marekani, linachunguza madai kuwa mmiliki wa klabu ya Los Angeles Clippers, Donald Sterling, alitoa matamshi ya kibaguzi .
Katika kanda iliyowekwa kwenye mtandao na sauti inayodaiwa kuwa ya bwana Sterling, anasikika akimwambaia mwanamke mzungu kutojionyesha hadharani na wenzake wamarekani weusi.
Shirikisho la NBA lilitaja matamshi yake kuwa ya kukera.
Wachezaji wake wanasusia kucheza baada ya ripoti kutokea kuwa mmiliki wa timu hiyo alirekodi matamshi ya kibaguzi kwa njia ya siri.
Wachezaji wa Los Angeles Clippers, walifanya mazoezi yao ya kujiandaa kwa mechi siku ya Jumapili wakiwa wamevalia jezi zao ndani nje ili kuficha nembo ya timu hio.
Shirikisho la kitaifa la mchezo huo, linachunguza taarifa kuwa mmliki wa Clippers Clippers, Donald Sterling alitoa matamshi ya kibaguzi.
Bwana Sterling aliambia mtandao wa TMZ kwamba matamshi hayo hayakuwa ishara ya msimamo wake.
Bwana Donald Sterling mmiliki wa timu ya Clippers
Clippers walikuwa wanacheza dhidi ya Golden State Warriors mjini in Oakland Jumapili. Katika mechi muhimu ya NBA, iliyozingirwa gumzo kuhusu hoja ya matamshi ya bwana Donald Sterling mwenye umri wa miaka 80 yaliyorekodiwa kisiri.
Wachezaji hao pia walivalia mikanda mieusi na soksi nyeusi pamoja na jesi zao za kawaida.

Je ni Bwana Sterling au siye?

Bwana Donald alinaswa akiongea kwa dakika kumi katika kanda iliyowekwa kwenye mtandao wa TMZ. Anasikika akimkosoa mwanamke mmoja mzungu aliyejipiga picha
na marafiki zake wamarekani weusi wakihudhuria mechi za Clippers.
Picha hio ilikuwa imewekwa kwenye mtandao wa kijamii.
''Inauma sana kwa mtu kutaka kujionyesha hadharani akijihusisha na watu weusi. Je ni lazima?'' anahoji bwana Donald.
"ninachoomba tu ni kutoiweka picha hiyo kwenye mtandao na pia kutaka wasije kwenye mechi zangu,'' aliongeza kusema bwana huyo.
Rais Barack Obama,amelaani matamshi hayo aliyosema yanakera na ya kijinga .
"wakati watu wajinga wanataka kutangaza ujinga wao, usifanye chochote , waacheni tu waongee,'' alisema Obama
Katika taarifa ya pamoja kwenye mtandao wa TMZ, Bwana Donald na maafisa wa Clippers walisema kuwa bwana Sterling amesikia sauti hiyo lakini hajui kama ni ya kweli au ikiwa imebadilishwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: