Meli ya Korea Kusini ikizama
Watu walionusurika kifo katika
ajali ya meli nchini Korea Kusini wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya
kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba,
ikiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama.
Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460. Zaidi ya miatatu hawajapatikana , wengine 164 wameokolewa na wengine wawili wamethibitishwa kufariki.
0 comments: