Uncategories
BINTI WA KIBONGO MWANA CHUO ASABABISHA MZUNGU KUFUKUZWA KAZI
BINTI WA KIBONGO MWANA CHUO ASABABISHA MZUNGU KUFUKUZWA KAZI
Raia mmoja wa nchini Finland amejikuta
katika wakati mgumu sana baada ya kushindwa kufanya lolote kazini
alipoajiriwa baada ya kutaka kuwa katika mahusiano na mwanadada huyu wa
chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye alimteka akili kiasi cha kumfanya
Mzungu huyo kuwa anashinda chuoni kutwa nzima kubembeleza akubaliwe
jambo lililomsababishia aache kuhudhuria kazini kwa muda wa miezi mine
mfululizo kutokana na kupagawishwa na uzuri wa mwanadada huyu ambao
umemfanya awe gumzo chuo kizima. Mzungu huyo ambaye ni muajiriwa wa
kampuni moja ya simu za mkononi (Jina limehifadhiwa) hapa jijini alikuja
Tanzania mwaka jana kwa dhumuni la kufanya kazi kwa mkataba amejitia
matatizoni baada ya kumtaka kimapenzi mrembo huyu ambaye alikutananae
kwa mara ya kwanza katika coffe bar moja iliyopo Mlimani city na
kwakushindwa kuzuia hisia zake alijikuta akiomba mawasiliano ya mrembo
huyu jambo ambalo ndio hasa limemsababishia matatizo kutokana na ukweli
kwamba Mzungu huyo amekuwa akimbembeleza sana mrembo huyu bila mafanikio
kiasi cha kumfanya aweanashinda Chuoni kwa huyu dada huyu Mlimani main
campas.
Utoro sugu wa Mzungu huyo umemuweka
katika wakati mgumu kwani amepewa barua mbili za onyo mpaka sasa na
amebakiza barua ya mwisho aachishwe kazi jambo ambalo mwenyewe anasema
kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwani hayuko tayari kumkosa dada huyo
licha ya ukweli kwamba nchini kwao ameacha mke na watoto.
Nilipomfanyia mahojiano dada huyo alidai
hawezi kuwa na mtu ambaye hana m,alengo nae ya muda mrefu kwani uwepo
wake hapa nchini ni wa muda mfupi tu hivyo yeye hayuko tayari kuwa kama
chombo cha starehe kwa kila mpita njia. Licha ya kumpongeza dada huyo
nilitaka nifahamu kama ameshamwambia ukweli Mzungu huyo ambapo dada
alieleza kuwa ukweli ameshamwambia lakini jamaa huyo amekuwa
king’ang’anizi kiasi cha kumnyima mpaka muda wa kujisomea jambo
linalomfanya akate shauri la kwenda kumripoti katika kituo cha polisi
kilichopo chuoni hapo endapo kesho siku ya kesho atathubutu kumfata tena
0 comments: