Mbunge mmoja ameuawa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Mogadishu Somalia.
Kundi la wanagmabo la Al Shabaab limekiri kufanya shambulizi hilo dhidi ya mbunge Isak Mohamed Rino.Wanajeshi wa serikali wameweza kupiga hatua dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab katika siku za hivi karibuni , lakini kundi hilo bado linadhibiti maeneo mengi ya Kusini mwa Somalia.
Waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed, amelaani shambulizi hilo na kulitaja kama kitendo cha uoga.
Rais Hassan Sheikh Mohamud mnamo siku ya Jumapili, alifungua rasmi kongamano hilo akisema kuwa tabia ya mashambulizi ya kiholela ambayo yamegubika Somalia kwa miaka 23 lazima ikome.
Kundi la Al-Shabaab hufanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia mjini Mogadishu na katika maeneo mengine ya nchi hiyo.
Somalia imekuwa ikikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 1991 wakati Siad Barre alipopinduliwa.
0 comments: