Friday, 18 April 2014

MKAKATI MPYA WA BUNGE/CCM KUHUSU KATIBA MPYA HUU HAPA



Nilipotea kidogo kuwapa habari za ndani kuhusu yanayoendelea ndani ya Bunge maalum la katiba. Jana kulikuwa na kikao cha kamati ya uongozi kujadili kuhusu kujitoa kwa UKAWA ndani ya bunge hilo. Katika kukabiliana na matokeo ya UKAWA kujitoa na mustakhabali wa katiba mpya kikao cha kamati ya uongozi kimedhamiria kufanya yafuatayo kwa siri kubwa:

Imekubaliwa kuwa mara baada ya bunge kuahirishwa wiki ijayo, serikali itaandaa marekebisho mapya ya sheria ya mabadiliko ya katiba ili kuondoa kipengere cha maamuzi kufanywa na rheluthi mbili ya wajumbe toka Bara na theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar.

Badala yake, kipengere hicho kitaeleza kuwa maamuzi yatafanywa na theluthi mbili ya wajumbe wa Bara watakaohudhuria kikao kitakachofanya maamuzi na rheluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar watakaohudhuria kikao kitakachofanya maamuzi. Ikumbukwe kuwa sheria kwa sasa inataka maamuzi yaridhiwe na theluthi mbili ya wajumbe wote (hata wasiohudhuria wanahesabiwa) toka bara na zanzibar jambo ambalo kujitoa kwa Ukawa kutaathiri maamuzi na hasa upande wa zanzibar.

Aidha kamati ya uongozi inaendelea na trick ambayo wapinzani walichelewa kuibaini hadi walipojitoa juzi ya kuweka 'majembe' yake kutoa hoja zao mwishoni mwa mjadala na kuwatanguliza wapinzani wote mwanzoni. Majembe ya ccm ni pamoja na Andrew chenge na Dr Migiro ambao ndio walioiandaa rasimu mbadala ya CCM. Hii inafanyika purposely jama alivyotangulizwa Warioba na JK akaja kufunga kazi huku UKAWA wakishindwa kubaini trick hiyo ya 'Save best for the last'. 

Ukawa na wapinzani sasa wakae tayari kwa marekebisho hayo ya sheria ambayo yamepangwa kuwasilishwa mwishoni kabisa mwa bunge la bajeti kwa hati ya dharula
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: