Wednesday, 16 April 2014

POLISI WATOA DAU KUBWA KWA ATAKAE SEMA NANI KALIPUA BOMU ARUSHA



Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza zawadi ya Tsh.Milion 10 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa wahusika walioshiriki mlipuko wa bomu lililolipuka Arusha,Bomu hilo lililipuka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye bar ya Arusha Night Park ambalo lilisababisha majeruhi kadhaa.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania Dci Isaya Mgula amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalam wa mabomu kutoka Jwtz na Jeshi la Polisi Tanzania umebaini bomu hilo limetengenezwa kienyeji mbali na hilo lililolipuka Jeshi la Polisi pia lilibaini bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba uliokua umeeegeshwa pembeni ya kiti kwenye bar jirani ya Washington
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: