Saturday, 12 April 2014

Utovu wa nidhamu wamponza Mourinho


Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho
Meneja wa timu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho ametozwa faini ya pauni £8,000 na ameonywa kuhusu mwenendo wake baada ya kutolewa nje katika mechi ya mwezi uliopita pale Chelsea ilipokubali kipigo cha Aston Villa cha goli1-0.
Mourinho alingia uwanjani katika kiwanja cha Aston Villa cha Villa Park kusema na mwamuzi wa mchezo huo Chris Foy baada ya kumpa kadi nyekundu mchezaji wake Ramires.
Mourinho amekana kosa la utovu wa nidhamu lakini ilithibitishwa katika tume huru iliyosikiliza mashitaka hayo Jumatano.
"Sijui ni kwa nini nilitolewa nje ," Mourinho alihoji baada ya mchezo.
"Niliuliza, lakini mwamuzi alikataa kuzungumza nami."
Mourinho alimshutumu Foy ada ya mchezo katika uwanja wa Villa Park katika matokeo ambayo yalisababisha Chelsea iliyokuwa ikiongoza ligi kuu ya England kupoteza pointi nne.
Ramires alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kumchezea vibaya mchezaji wa Aston Villa, Karim El Ahmadi, kitendo kilichosababisha vurugu kiasi.
Mourinho anadai kuwa alikuwa akijaribu kuzungumza na Foy kwa sababu Ramires alisukumwa na mshambuliaji wa Villa Gabriel Agbonlahor, ambaye alibadilishwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: