Mshirikishe mwenzako
Shambulizi hili linadaiwa kufanywa na Boko Haram ingawa
kundi hilo halijakiri kulitekeleza
Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni ya
wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini
Mashariki mwa nchi hiyo huku wasichana wakitekwa nyara.
Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili
wametekwa nyara na washambuliaji hao.
Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la
wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram. Utekaji nyara huo
ulifanyika usiku wa manane katika shule ya Chibok ksuini
mwa mji wa Borno , karibu na mpaka na Cameroon.
Inaarifiwa wasichana 300 walikuwa
wanajiandaa kwa mitihani yao. Mmoja wa
wasichana alifanikiwa kutoroka na aliambia
BBC kuwa walikuwa wanalala wakati
walipovamiwa na wanaume waliokuwa
wamejihami.
Waliowashambulia wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi
la Boko Haram.
Wanaume hao waliingiza magunia ya chakula katika malori
yaona kuwaamuru wasichana kuyapanda malori hayo.
Wasichana 15 walifanikiwa kutoroka baada
ya lori walimokuwa kukumbwa na hitilafu.
Wakazi wa kijiji cha Chibok wanasema kuwa walisikia
milipuko kadhaa huku nyumba 170 zikiteketezwa.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi
wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi
hilo mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa
katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi
mjini Abuja.
Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya
shambulizi hilo.
0 comments: