Habari za Jumapili mdau wa GK, leo katika kipengele chetu cha chaguo, kwa mara nyingine tumekuchagulia wimbo uliowika mitaa ya jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake miaka takribani mitatu iliyopita. Safari hii ikiwa ni maalumu kwa ajili ya tukio muhimu la mwimbaji wa wimbo huu ambao unaitwa'Tutembelee' kutoka kwa bwana harusi wa leo kijana Lembo Junior Emanuel ambaye anafunga ndoa alasiri ya leo na Anna Fisoo katika kanisa la TAG Tabata Kisukuru jijini Dar es salaam.
Wimbo huu umebariki maisha ya wengi, ambao wameita uwepo wa Mungu katika maisha yao. Natumaini, itakuwa hivyo hata kwako hii leo endapo utaliita jina la Mungu na kumwambia akutembelee katika kila jambo na nafasi uliyonayo, hakika utakuwa umeyaweka maisha yako sehemu salama na yenye uhakika. Tunakutakia jumapili njema yenye baraka.
0 comments: