Saturday, 17 May 2014

MUUJIZA: MAMA AKUMBATIA MAITI YA KICHANGA CHAKE HADI KIKAFUFUKA

Kate na Davie Oggs wakiwa na kichanga chao. ©Howlifebegan/youtube Hakuna furaha kubwa kwa mjamzito kujifungua salama, mtoto aliye na afya njema. Na hakuna majonzi makuu kwa mjamzito kupoteza kichanga chake kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kuibiwa ama kufuariki. Kilichotokea kwa mama huyu huko Sydney, (Autsralia) anayefahamika kwa jina la Kate hakika hakielezeki kwa urahisi. Akiambatana na mume wake, Daid Ogg - walifika hospitalini hapo ambapo mama huyo alijifungua watoto mapacha kabla ya muda muafaka, ambapo walikaa tumboni kwa kipindi cha miezi 6 tu. Pacha wa kike, Emily alinusurika, wakati pacha wa kiume, Jamie, alitangazwa na daktari kuwa amefariki punde tu baada ya kuzaliwa. Katika hali ya majonzi, mama wa kichanga hicho, Kate - alishika mwili wa kichanga chake hicho, huku akikiongelesha pamoja na mumewe licha ya kwamba walishafahamishwa kuwa hauna uhai (a lifeless body) - kwa kukitajia jina la dada yake, na kwamba anaendelea vizuri, huku pia wakimuita kwa jina lake (japo hasikii). Tazama Video wakihojiwa na kituo cha MSNBC Kwa masaa mawili wazazi hao waliuongelesha mwili wa kichanga hicho ambacho hakikuwa na pumzi, na baada ya muda huo kila mtu akabaki ameduwa baada ya kichanga hicho kufungua macho na kuungana na familia hiyo ambayo ilijawa na furaha ya ajabu, ambapo wanaeleza tukio hilo kwamba si kingine bali ni muujiza. Hakika hapo pia tunakumbushwa kuwa maneno yana nguvu ya kuumba ama kubomoa, jambo gani unalisema kwa mtoto wako ama mwenza wako? Mjenge kwa namna ambavyo anatakiwa kuwa, ikiwemo kumpa jina zuri na sio kumsema kwa namna alivyo. Uliwahi kusoma taarifa ya kichanga ambacho kilifufuka baada ya maombi? Bofya hapa kuisoma taarifa hiyo. Tukio hili ambalo lilitokea nchini Australia mnamo mwaka 2012, limeibua imani kwamba chochote kinawezekana iwapo mtu hatotilia shaka. Katika kuhojiwa na kituo cha MSNBC, wazazi wa mapacha hao wanasema kwamba hawakutarajia kitu kama hicho, na kwamba hata madaktari mwanzoni walipoelezwa walisema kuwa hisia zao tu kwa kuwa mtoto amekwishafariki.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: