KWA TAARIFA YAKO: WAIMBAJI WANAOTOKA UKOO MMOJA TANZANIA, BARAKA YA SAUTI MUNGU AMEWAPA
published on 22:26:00
leave a reply
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Mwanamama Upendo Nkone, ama mwite mama Askofu Mbeyela.
KWA TAARIFA YAKO hii leo mdau wa GK tunaanza namna hii "Heri mzigo wa mabeganii kuliko moyoniii, ukisema utulie upumzikee maumivu huzidiii, mawazo huongezeka moyoniii hakuna amani, zaidi wasiwasi huzidii sababu ya dhambii, dhambi ni mzigo ooo huchokesha moyoo, dhambi ni mzigo ooo huleta huzunii, dhambi ni mzigo oo huzeesha mapemaa, dhambi ni mzigo oo kimbilia kwa Yesu" Hayo ni baadhi ya maneno ambayo yanapatikana katika wimbo dhambi ni mzigo ulioimbwa na mchungaji David Nkone mmoja wa waimbaji kutoka katika ukoo wa akina Nkone ambao GK inathubutu kusema kwamba imebarikiwa kwakuwa na waimbaji haswa na walioitwa kwenye huduma.
KWA TAARIFA YAKO ukoo huu unawaimbaji mbalimbali kuanzia kwakina baba, akina mama, mashangazi, wajomba na wengineo ambao wapo kwenye kwaya mbalimbali wakisukuma sauti zao bila kujulikana lakini Upendo Nkone ama mama askofu Mbeyela ndiye anajulikana zaidi katika ukoo huo. Kwa leo GK inakutajia
Mchungaji David Nkone.
wachache ambao inawajua wa kwanza ni mchungaji David Nkone ambaye bado anaimba na anapatikana nyumbani kwao huko mkoani Kigoma, kuna mchungaji Donis na mkewe Nnunu Nkone ambao licha ya kuhubiri pia ni waimbaji wakimtangaza Kristo huko nchini Marekani ambako wameweka kambi.
KWA TAARIFA YAKO kuna mchungaji Huruma Nkone yeye yupo jijini Dar es salaam akichunga kanisa la Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) lililopo Mbezi, lakini pia kuna mwanadada aliyetamba vyema na kwaya ya The Reapers ama wavunaji kutoka Kimara KLPT aitwaye Dissa Nkone akiimba nyimbo kama Haja ya moyo wa mwanadamu, Tanzania, Ninaye Rafiki, Ninakuhitaji Roho na nyinginezo, lakini pia kama haitoshi kuna mwimbaji mwingine ambaye hata hivyo GK haijapata jina lake kamili anaimbia kwaya ya Dar es salaam Gospel choir (D.G.C) ya Kurasini FPCT ambaye hata hivyo bado hajaamua kushika kipaza sauti na kuongoza nyimbo.
Mchungaji Donis na Nnunu Nkone.
KWA TAARIFA YAKO hao ni baadhi tu ya waimbaji na wahudumu walioitwa kumtangaza Kristo kupitia ukoo wa akina Nkone kutoka pale mkoani Kigoma, lakini pia wapo wengine kama GK ilivyosema kuna dada anaitwa Dafroza Nkone uimbaji wake ni wakipekee, kuna mwingine anaitwa Delaya ambaye hapana shaka ndiye mkubwa taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba alikuwa anasali Full Gospel kwa askofu Zachary Kakobe hapana shaka bado yupo huko, huyu naye ni hivyo hivyo kama ndugu zake wengine. KWA TAARIFA YAKO wanandugu hawa wamekuwa baraka kila eneo ambalo wanatumika katika kumuinua Mungu. Lakini pia kama mwanzoni GK ilivyokupasha hawa ni wachache tu ambao inawafahamu lakini pia kuna wajukuu, watoto, na wengine ambao pia ni waimbaji katika ukoo huu wa akina Nkone.
KWA TAARIFA YAKO ukoo huu si kwamba ni ukoo pekee ambao upo kwenye uimbaji la hasha kuna koo nyingine nyingi zinazojulikana na zisizojulikana ingawa nyingi zao zimejikita kwenye kwaya ambako utakuta baba mpaka watoto wake wanaimba kwaya moja ama mbalimbali. Moja wapo ya familia nyingine ni ya marehemu Canon Mtangoo ambaye watoto wake ni waimbaji na wapigaji muziki wa kwaya maarufu nchini ya Tumaini Shangilieni Arusha.
Dissa Nkone.
KWA TAARIFA YAKO Ukitaka kupata album ya mchungaji David Nkone inayoitwa 'Mimi ni Msafiri' yenye wimbo wa dhambi ni mzigo piga simu namba hii +255 655 929 669,757 929 669, utapewa maelekezo namna ya kuipata CD ya nyimbo hizo. Ukitaka kusoma mapito aliyopitia Upendo Nkone BONYEZA HAPA
Mchungaji Huruma Nkone.
0 comments: