Tuesday, 13 May 2014

Dr.Cheni Asikitishwa Na Habari Za Kuzushiwa kifo.

Dr.Cheni alipokuwa amelazwa hospitali kala ya kuruhusiwa kutoka
Wiki iliyopita star wa muda mrefu katika tasnia ya filamu nchini Muhsin Awadhi "Dr.Cheni" alidaiwa kulazwa kutokana na kuumwa homa ya Dengue hata hivyo alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani ila baadhi ya watu wakaanza kuzusha maneno kuwa amefairiki. Kupitia Instagram Dr.Cheni alikanusha haabri hizo na kuonekana kusikitishwa na watu waliofanya kitendo hicho. "Jamani  kifo kipo na hakuna atakaye kwepa ni lazima tutakufa na hakuna atakayebakia ila si vyema kunizushia siku yangu itafika tu na nyote mtajua lakini si jambo la busara kunizushia.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: