Tuesday, 13 May 2014

Ray, Irene Uwoya, JB Na King Majuto wameenda Uturuki Kikazi

JB na Irene Uwoya
Wakiwa katika press conference
Ray na King Majuto
Mastaa wa filamu nchini King Majuto, Irene Uwoya, Vicent Kigosi "Ray"na Jacob Stephen(JB) w
anatarajia kuondoka Tanzania usiku huu kwenda nchini Uturuki kwa ziara maalum ya kikazi ambayo imedhaminiwa na Princess Casino iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam na wamiliki wenye asili ya Uturuki. Wsanii hao wakizungumza na media leo walisema kuwa kwa mujibu wa wenyeji wao watakutana na mastaa wa filamu na watu muhimu nchini humo na kujifunza tamaduni zao na pia kukuza wigo zaidi wa kazi za filamu za Tanzania. Ziara hiyo ni ya wiki moja.

Hili ni jambo jema kwa wasanii wetu kuonyesha kuwa tasnia na wasanii wetu wanatambulika. Pia ni matumaini yetu kuwa wasanii hawa wataenda kuutangaza utamaduni wa Tanzania nchini humo na sio wao kujifunza utamdun i wa nchi hiyo pekee.

picha na video kwa hisani ya Bongo5
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: