Jeshi la Nigeria limesema linajua mahali walipo wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram ila hawatojaribu kuwaokoa.
Mkuu wa Ulinzi nchini Nigeria alisema kuwa hizo ni taarifa nzuri kwa wazazi, japo alikubali kuwa jeshi halitoweza kuhatarisha kutumia nguvu.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na watu wenye silaha wa Boko Haram kutoka shuleni kaskazini mwa Nigeria mwezi Aprili.
Hapo awali BBC walitegemea kuwa mpango wa kuachiwa kwa baadhi ya wasichana ungefanikiwa ila uliahirishwa na serikali.
Mwandishi wa BBC Will Ross aliyeko mjini Abuja alisema mpatanishaji alikutana na viongozi wa kundi hilo la Kiislamu na kutembelea mahali waliposhikiliwa wasichana hao.
Anasema makubaliano yalikaribia kufikiwa ili kuachiwa kwawasichana 50 kubadilishana na kuachiwa kwa wafungwa 50 wa Boko Haram.
Ila serikali ya Nigeria ilisitisha mpango huo baada ya Rais Goodluck Jonathan kuhudhuria mkutano unaohusu mgogoro huo mjini Paris. Sababu za kujitoa bado hajizajulikana.
Nchi ya Nigeria ipo katika presha kubwa ya kufanya jitihada zaidi za kupambana na kundi hilo ili kuwaokoa wasichana hao.
Maelfu ya watu wameuawa tangu Boko Haram walipoanza kampeni za kihalifu dhidi ya serikali ya Nigeria mwaka 2009 na kuondoa hali ya usalama.

0 comments: