KOCHA
Didier Deschamps amefungua kesi dhidi ya demu wa Samir Nasri aliyemtusi
mwalimu huyo baada ya kutaja kikosi cha Ufaransa cha Kombe la Dunia
bila kiungo huyo anayechezea Manchester City.
Anara Atanes aliposti kwenye Twitter- matusi haya; "F*** France and F*** Deschamps! What a s*** manager".
Lakini ingasa baadaye aliomba radhi, Deschamps atachukua hatua za kisheria dhidi ya Atanes.
Kituo
cha Redio cha Ufaransa, RMC mimeripoti kwamba Deschamps na Shirikisho
la Soka Ufaransa (FFF) wore wamefungua kesi dhidi ya Atanes, ambaye ni
mzaliwa wa England na mwimbaji wa kundi la Pop, Fanfare.
0 comments: