Wakati diamond akiwa anasubiriwa kwa hamu sana huko nchini uingereza,
alipokuwa anatarajia kushusha bonge la show kali ya kihistoria usiku wa
jumamosi at the rugby 7s after party, na baada ya muda ilisemekana
kuhairishwa kwa show hiyo, huku Diaond akiomba msamaa kwa mashabiki wake
waishio huko nchini Uingereza kwa kuahirishwa kwa show hiyo, huku
akidai kuwa ni kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika.
Ila habari kutoka kwa mtu wa karibu sana wa Dangote(Diamond) aliyekuwa
anafuatilia mchakato mzima wa show hiyo, alifunguka hivi karibuni kwa
kile kilichomsibu Diamond hadi kuahirisha show hiyo;Diamond inasemekana
ndiye aliyechelewa kupeleka maombi ya Viza ya kusafiria, Viza hiyo
aliyoombwa kupitia Ubalozi wa Uingereza ulioko huko nchini Kenya, na
kwa kipindi ambacho kilichukua hadi taratibu zote zikamilike, na hadi
Diamond anafikishiwa Visa yake Bongo, mda ulikuwa ushapita na hakuweza
kwenda tena na kuweka mipango kama ilivyokuwa hapo awali, hadi mwisho wa
siku kupelekea kuahirishwa kwa show hiyo.
0 comments: