Wednesday, 14 May 2014

ORODHA YA WASANII WA KILI MUSIC TOUR 2014 YATAJWA, TWEET YA JAYDEE YAMPONZA, AACHWA MWAKA HUU



Orodha ya wasanii watakaoshiriki kwenye Kili Music Tour 2014 imetangazwa leo.
 
Mwaka huu zaidi ya wasanii 30 watashiriki katika ziara hiyo kwenye mikoa zaidi ya 10 nchini  itakayoanza Mei hadi Septemba 2014. Wasanii hao ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz, Linex, Proffesor Jay, Izzo Biznes, Kala Jeremiah, Fid Q, Snura, Weusi, Ben Pol, Mzee Yusuph, Shilole na Mwasiti.
 
Wengine ni Nay wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Juma Nature, Warriors From the East, Madee, Young Killer, Jambo Squad, AY, Vanessa Mdee, Mashujaa Band, Rich Mavoko na Christian Bella.
 
Hata hivyo Lady Jaydee aliyekuwepo kwenye ziara hiyo mwaka jana, ameondolewa mwaka huu.

Chanzo kimoja kimeiambia Mpekuzi  kuwa  sababu  ya  kuondolewa  ni ile  tweet ya dharau aliyoiandika Lady Jaydee kuhusu kutokufahamu kama tuzo hizo zilifanyika.
 
Chanzo hicho kimesema pia kuwa Roma alikuwa awepo kwenye ziara hiyo lakini ujuaji wake umemfanya apigwe chini.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: