Muigizaji mkongwe wa filamu za Kiswahili, King Majuto amekuwa mmoja kati ya wasanii tisa walijumuishwa katika safari ya kwenda matembezi nchini Uturuki ambayo imekuwa organized na JB.
Akiongea katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm, King Majuto amemshukuru JB kwa kumfikiria na kumpa nafasi hiyo kwa kuwa hakuwa na matarajio yoyote ya kufika Asia/Ulaya hivi karibuni.
Muigizaji huyo ameeleza kuwa endapo akipata mchongo wa kuigiza huko Uturuki atafanya hivyo kwa kuwa anafahamu kuongea kiingereza vizuri.
“Nashukuru kwamba nazungumza kiingereza vizuri, kwa hiyo hata nikipata actors/actress au nikipata kampuni ya uturuki ya kucheza cinema wakasema wanataka kucheza filamu na mimi ntafanya. Kwa hiyo namshukuru sana JB kwa sababu ananikumbuka sana Yule mwanangu. Namshukuru JB na Mkewe pamoja na Uwoya kwamba niwe nao. Nilikuwa sijui hii safari, wangeweza kuondoka wenzangu bila kunambia lakini nashukuru Mungu wananipenda.” Amesema Majuto.
Ameeleza kuwa angependa safari hiyo iwe sehemu ya kuijengea heshima Tanzania na kwamba Mungu akipenda wapate nafasi ya kujitangaza na kucheza filamu hata na waigizaji wa Uturuki.
0 comments: