Saturday, 24 May 2014

Mastaa Wa Hollywood Kumkoma Wema Sepetu Kwenye BET Awards 2014, Apanga Kuwafunika Kwenye Red Carpet !

Wema Sepetu in Eve Collections at Kili Awards 2014.
Habari mpya ni kuhusu Wema Sepetu kuhudhuria tuzo za BET Awards 2014 ambazo zimepangwa kufanyika hivi karibuni huko Los Angels marekani na kuwakutanisha mastaa wa Hollywood wakiwemo wanamuziki na mastaa wa filamu. Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema ambaye umaarufu wake ni mkubwa Tanzania kuliko hata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini kikizungumza na Swahiliworldplanet leo kimesema kuwa Wema anajiandaa vilivyo kwenda kufunika mastaa wa Hollywood katika red carpet ya BET Awards 2014 ambapo mpenzi wake Diamond Platinumz amependekezwa kuwania tuzo ya Best International Act, Africa. "nakupa exclusive, Wema anaji-prepare kwa ajili ya tuzo za BET Awards 2014, siwajua Nasib(Diamond) anawania tuzo hizo, basi Wema atatia team ninavyokuambia ana hakikisha muonekano wake kwasasa hauna hata kipele cha joto siwajua tena atakutana uso kwa uso na kina Beyonce na Rihanna ! basi ataka kuwaonesha kazi kuwa kuna mademu wakali toka Bongo ha ha ha haaaa(akiangua kicheko)............chonde chonde usije ukaniandika jina langu blogini" kilisema chanzo hicho ambacho pia ni msanii wa filamu

Chanzo hicho kilipoulizwa kuwa je wataenda Wema na Diamond pekee au na mama Diamond pia ataenda kumsapoti mwanae kilisema kuwa mama Diamond anaweza kwenda kuosha nyota pia lakini Diamond ataondoka na maneja wake kwa anavyojua kwasasa " hilo sina uhakika kwa sasa ila nitakujuza usijali but Diamond na Wema wataenda na management ya Diamond siwajua ni tukio international, pia Martin Kadinda(meneja wa Wema) anaweza kwenda"

Alipoulizwa anadhani Wema Sepetu atavaa nini kwenye red carpet alisema hajui na hayamhusu hata akivaa gunia shauri yake lakini mbunifu maarufu nchini Evelylin Rugemalira(Eve Collections) ana uwezekano mkubwa wa kumvalisha sababu ndiye anayemuwezea kwenye red carpet nyingi ikiwemo tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 Wema alikuwa kama showstopper "sijui hilo hata akivaa gunia it is none of my business kikubwa jua ataenda but kuna yule dada wa Eve Collection nafikiri unampata basi yule anaweza kumvalisha Wema, Nakwambia mastaa wa Hollywood watamkoma......sisi yetu macho tunasubiri picha mtuwekee" kilisema chanzo hicho chenye maneno mengi

Hata hivyo jana kupitia Instagram Wema aliandika post kuashiria atahudhuria tuzo hizo kwa kusema...
                                                            Wema na Diamond
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: