Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Morogoro na baadaye kuokolewa na polisi.
Mwenyekiti
wa Bavicha, John Heche akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa
kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la
Kalenga, lringa.
Mmoja
wa viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro, lnnocent Zawadi ambaye
alikuwepo jimboni Kalenga naye akithibitihsa pia kumtambua kijana huyo.
NJEMBA mmoja amepokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa Ukawa
waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jana Jumatano jioni baada ya
kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge wao, Rose Kamli wakati wa
uchaguzi mdogo jimboni Kalenga, mkoani Iringa.Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo kikali baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki katika kumteka mbunge wao na kumpiga kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa mwezi uliopita.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
0 comments: