Nyoka hao wana uzito wa kilo 250 na mtu anayefanyiwa massage anaweza kupiga kelele au hata kupumua bila nyoka hao kufanya chochote.
Unaweza usifikirie kama kuna kitu kama hiki kinafanyika lakini mbuga hii iliyopo katika mji wa Cebu nchini Ufilipino inapata wateja wengi sana wakipanga foleni kusubiri huduma ya kukandwa mwili “Massage” ambayo hutolewa bure lakini kwa wanaoweza tu kuhimili mikiki yake.
Nyoka hao wakubwa wanne waliopewa majina ya Michelle, Walter, EJ and Daniel hutolewa nje kutoka kwenye eneo wanapofugwa na kuwekwa juu ya mtu anayetaka huduma huyo wakati mtu huyo akiwa amelala chini kwenye kitanda maalum karibu na lango kuu la kuingilia katika mbuga hiyo.
Watu wengi wanashangazwa na mbuga hii na huduma inayotolewa sasa jiulize unaweza kufanya hivyo hata kama una uchovu kiasi gani?
Story hii na nyingine zote millardayo.com ipo tayari kukufikishia kwa wakati popote ulipo, kaa karibu yangu kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook ili kupata kila kinachonifikiwa ikiwemo pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.
Niachie comment hapa chini… uko tayari kwa hii massage?
0 comments: