Kama wewe ni mfuatiliaji wa mieleka lazima jina la Hulk Hogan unalifahamu hata hauhitaji ushahidi wa picha zake, mbabe aliyesumbua ulingo wa mieleka kwa miaka mingi.
Jaji wa mahakama ya Los Angeles ametoa amri ya kuwataka rafiki wa zamani wa Hulk Hogan aitwae Bubba na mkewe wa zamani wa mwanamieleka huyo Heather Clem kupeleka mkanda au video ya ngono inayomuonesha mwanamieleka huyo akibanjuka na mkewe huyo wa zamani.
Sababu za jaji huyo kuomba aletewe video hiyo ya pilau ni kutokana na kuwepo kesi nzito iliyofunguliwa na mwanamieleka huyo akidai kuwa video hiyo ilivujishwa kwenye mitandao na wawili hao na kwamba walimchukua bila idhini yake.
Mwaka 2012 Hulk Hogan alifungua kesi dhidi ya mkewe huyo wa zamani na rafiki yake kwa kitendo walichomfanyia huku akidai fidia ya $100 million kutoka kwa mtandao uliopost video hiyo.
Pamoja na filamu hiyo ya ngono, jaji amewataka Bubba na Heather kuwasilisha pia messages zozote za siri walizopokea baada ya kuvujisha video hiyo mtandaoni.
0 comments: