Taarifa zinadai mwanamke asiyejulikana, huenda akawa ni Bi. Lewthwaite, alisindikizwa na polisi kwenda kuitembelea kambi ya jeshi la Kenya iliyopo Somalia kabla ya kutoweka.
Mwanamke huyo anashitakiwa kwa ushirikiano na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, ambalo limeishaishambulia Kenya mara kadhaa.
Mume wa Bi. Lewthwaite alifariki kwenye shambulio la kujitoa mhanga mwaka 2005.
Mume wake Germaine Lindsey alikuwa ni mmoja kati ya watu wanne waliolipua mabomu Julai 7 mjini London na kuua watu 52 na kujeruhi mamia mwaka huo.
0 comments: