Staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.”Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
0 comments: