Thursday, 17 July 2014

MABIBI NA MABWANA NAKUALIKA KUTAZAMA VIDEO MPYA YA LINAH – OLE THEMBA.

Wiki chache Linah alianza kupost vipande vya picha na video ambayo wengi tulikua tukiona tu maandishi yanayosema inakuja,leo baada ya futari THT Linah ameitumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi video na audio ya wimbo huu. Mtu wa kwanza kuinunua video hii ambaye ameingia kwa rekodi ni Cloud kutoka Bongo Movie ambaye alipoiona tu akatoa pesa akainunua,wapili ni Mrisho Mpoto ambaye nae hakutaka kusubiri zaidi. Linah ameagwa rasmi na uongozi wa THT baada ya kupata uongozi mpya utakaoanza kumsimamia kazi zake ambazo kwa utangulizi wameanza na kazi hiyo iliyofanyika South Africa kuanzia audio hadi video na kampuni hiyo inaitwa No Fake Zone Entartainment.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: