Khadija Kopa amefunguka na kusema kuwa baada ya mume wake kufariki na muda kupita itambidi aolewe tena maana hawezi kuwa mzinifu hivyo atafuata taratibu za imani yake na kufunga ndoa ili awe mke halali na aepuke uzinifu.
Mbali na suala la kuolewa Malkia wa mipasho amekana tuhuma zilizopo mtaani kuwa anapenda sana dogo dogo maarufu kama Serengeti Boys na kusema kuwa yeye anampenda mtu anaempenda na yule ambae anakuwa na makubaliano nae tena kwa maelewano na si kama ambavyo watU wanakuwa wakisema kuwa anatoka na watoto wadogo.
0 comments: