Thursday, 17 July 2014

JOSHUA NASSARI ASHIRIKI MDAHALO WA VIONGOZI WADOGO BARANI AFRIKA NCHINI MAREKANI.


Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akizungumza wakati wa mdahalo wa viongozi wadogo wanaoshiriki programu ya rais Obama kwa viongozi wadogo wanaoonyesha dira .Mdahalo huo umefanyika katika chuo kikuu cha Arkansas ambacho Rais Mstaafu wa Marekani  Bill Clinton na mkewe Hillary walianzia kazi ya kufundisha Sheria.
Baadhi ya washiriki katika mdahalo huo ambamo miongoni mwa waalikwa walikuwa ni watanzania waishio Arkansas.
Mkurugenzi wa program ya Rais Obama ya "Young African Leaders initiative "(YALI) Dr, Leyah akizungumza katika mdahalo huo uliobeba kichwa cha "BRINGNG THE GAP BETWEEN THE DIASPORA AND OUR HOME COUNTRIES".
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza muda mfupi baada ya kutembelea makao makuu ya shirika la Heifer International ambalo limetoa ahadi ya kuendelea kusaidia jamii hususani katika elimu na mitaji huku likitoa mradi wa Ng'ombe wa maziwa kutoka kwa jimbo la Arumeru Masharik


Mbunge jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nssari akila pozi la picha na mratibu wa kijiji cha Heifer ,Bi Hellen Brown .
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari pia alipata nafasi ya kushiriki mahojiano juu "vijana na mustakabali wa Afrika"katika kituo cha Luninga cha Umma kinachojulikana kama Fayetteville Public  Access Television.shoto ni mwandishi wa kituo hicho Dan,Prof Mitiku toka chuo kikuu cha Makelle nchini Ethiopia,wote hawa wanashiriki program ya Rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na mshiriki mwenzake katika programu ya rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika inayofanyika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani ,Bi Clara toka nchini Nigeria ambaye pia ni balozi wa UN Charter nchini Nigeria.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: