Wednesday, 16 July 2014

MAHUSIANO: ALAMA ZA KUKUONYESHA KUWA SASA MPENZI WAKO ANAKUACHA YA KWANZA HII HAPA



Hakuna anaeweza kukili kuwa hateswi na mahusiano ya mapenzi sii mwalimu au mzazi wala meneja hata mkurugenzi lakini mapenzi yatawala dunia nzima sasa tujifunze hili kidogo

1. AKIKWAMBIA ANAHITAJI NAFASI:
 
Hii sio dalili nzuri kikawaida kama mko kwenye mahusiano
Kwasababu nyie wawili mmekubaliana kwamba kila mmoja anavutiwa na mwenzi wake na mko tayari kutumia muda wenu pamoja . 
Lakini boyfriend/girfriend anaehitaji nafasi ya peke yake si mtu ambae anataka kuwa na wewe kwa muda mrefu......Chapa lapa 
 ANAHITAJI NAFASI ? YA NINI ? KWANI UKIWEPO UNAMNYIMA HEWA? 

Kama unahitaji alama moja tu ya kukuonyesha kuwa mtu hakutaki ...this is it. 
Ni kama anakwambia indirect kuwa hahitaji kukuona. 
Haka ka kipande ka kusema, “I need space” ni mbinu ya kutafuta mlango wa kutokea...

Pengine anasema hivyo ili asikuumize sana,
Hebu fikiria mtu akwambie bwana eeh sikutaki, 
Au akwambie kwa sasa naomba tusionane kuna mambo nafanya nitakutafuta nikiwa na muda,,,, kipi kitakuuma zaidi??  Binadamu tunapenda kudanganywa hivyo uongo unatupa faraja na ukweli unaumiza.

Sasa ndugu ukiona hizo dalili kuliko usubiri hadi uachwe bora uchape lapa tu ujidai na wewe ulikuwa unahitaji space pia, kikakuume mbele kwa mbele bila yeye kujua.
Mtu anajidai anahitaji space saa hizi, wakati mnaanza hakuiona hiyo space? 
Mpe space kabla hajaiomba, jiwahi kabla hujaachwa

SULUHISHO:
 
Ila kama unaweza kurekebisha jaribu kuangalia matatizo madogo mdogo ambayo wewe na mwenzio pengine mmekuwa mkikumbana nayo kwa muda bila suluhu, 
Na pia angalia kama mnaweza kuyamaliza kwa kuzungumza na kurekebisha penye madhaifu kabla ya kuachana

Ila mambo makubwa ya kujiuliza wakati unajaribu kuokoa mahusiano mi kama haya:
1.Je! mahusiano hayo unayahitaji kweli? na je yana thamani ya kuokolewa ? Au uko desparate tu ilimradi uwe na mtu?

2.Pia angalia kama mwenzio nae yuko tayari kurudi,? ili isiwe wewe tu ndio unalazimishia

3.Uhusiano wa mapenzi upande mmoja ni mateso bila chuki

4.Tafuta muda mkae wawili muambizane ukweli, mtoe dinner au mpeleke sehemu anayoipenda

Maana kuachwa si jambo dogo, na si rahisi kulibeba
Ni bora ujiandae ujue kabisa unaachwa kuliko uwe kama kipofu mpk uguswe eeeh jamaa kaenda
Ukijizatiti hata moyo unakuwa hauumi sana
Wazungu wanasema

If you can read signs, you will be better equipped for dealing with getting dumped.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: