Chege Chigunda anatarajia kuachia album yake mpya ambayo bado inaendelea kupikwa na tayari nyimbo nane zimekamilika.
Chege
Chege ambaye anajipanga kwenda Kenya hivi karibuni kwaajili ya kwenda kufanya kazi na Nonini, ameiambia Bongo5 kuwa safari ya Kenya ndo itasimamisha kwa muda kazi ya kurekodi album.
“Album yangu binafsi inakamilika soon, tayari nimesharekodi nyimbo nane na bado ninaendelea. Sema kuna kazi naenda kufanya Kenya na Nonini, Nonini featuring Chege. Pia licha ya Nonini pia kuna kazi nyingine nitaziweka wazi pindi zitapokamilika. Kwahiyo nikiridi Kenya nitamalizia na baadaye itatoka,” alisema Chege.
0 comments: