Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba ya ufunguzi wa
Maonesho ya Muziki katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani jana ambayo
hufanyika kila mwaka samba mba na utoaji wa Zawadi kwa mwaka 2015
pia kujumisha wanamuziki na wasanii mashuhuri kutoka nchi za Afrika na
nchi mbali mbali Duniani.[Picha na Ramadhan Othman,]
Baadhi ya washiriki katika
ufunguzi wa Maonesho ya Muziki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa
hutua yake jana katika viwanja vya maonesho ya muziki yanayofanyika
katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani sambamba na utoaji wa zawadi
kwa mwaka 2015 akiwa katika ziara ya kikazi ,
KIkundi cha Matona kutoka Zanzibar
kilipokuwa kikitoa burudani yake wakati wa Tamasha la Maonesho ya
Muziki wa Kiafrika yanayojumisha wasanii na wanamuziki mbali mbali
kutoka Afrika na Mabara mengine Duniani wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein alihudhuria
akiwa mgeni rasmi katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini
Ujerumani,
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein akitunza wakati Kikundi cha Matona kutoka Zanzibar
kilipotoa burudani wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya Muziki
yanayofanyika jana katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akijumuika na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein katika ziara ya kikazi pamoja na ujumbe wake, maonesho hayo
yameshirikisha Nchi za Afrika na Mabara mengine Duniani,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkwewe Mama Mwanamwema Shein
(katikati) wakiwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Utalii na Michezo Said
Ali Mbarouk (wa nne kushoto)na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya
Mzee (wa pili kulia) na watayarishaji wa Maonesho ya Tamasha la Muziki
katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani lililofunguliwa jana.
0 comments: