Taharuki imetanda mjini Kampala Uganda baada ya habari kuenea kuwa mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ,aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi anarejea leo.
Inadaiwa kuwa polisi wametumwa katika barabara ya kutoka Kampala hadi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
Bwana Mbabazi anasemekana kuwa anarejea kutoka kwa ziara ya kimataifa
iliyompeleka Uingereza na Marekani huku wafuasi wake wamepanga
kumkaribisha kwa shangwe na vigelegele.Pamoja na msafara wa magari
yaliyojaa wafuasi wake kumkaribisha.
Amama Mbabazi alitangaza majuma mawili nia ya kushindana na rais
Museveni kuwania uwenyekiti wa chama cha National Resistance Movement na
hatimaye kuwania kiti cha urais.
0 comments: