Siku chache zilizopita tulishuhudia Marekani wakihalalisha ndoa za jinsia moja kwenye majimbo yao yote, lakini hali haiko hivyo ndani ya China, ndoa za jinsia moja kwao zinakatazwa japo inaonesha wapo wanaotamani kuona hali hiyo inabadilika.
Stori nyingine kutoka China inahusu wanawake wawili wanaoishi Beijing, Li Tingting na Teresa Xu wameingia kwenye record ya kitu tofauti, wamefunga ndoa siku ya Alhamisi wiki iliyopita.
Wawili hao ni wapenzi wa muda mrefu,
waliamua kufunga ndoa hiyo na kufanya sherehe kubwa iliohudhuriwa na
watu zaidi ya 50, sherehe hiyo ilifayika kwenye moja ya Hoteli kubwa
katikati ya Beijing.
Wanandoa hao walisema waliamua kufanya maamuzi hayo baada ya kuona Marekani wameruhusu ndoa za aina hiyo… wamesema walikuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu wakaona time hii waingie tu kwenye ndoa.
>>> “Tunajua
sheria za nchi zinakataza, lakini kama Marekani wameweza kutambua kuwa
hata kundi la watu kama sisi tunastahili kutambulika kisheria hatuoni
sababu ya kwa nini watu waliopo huku wanyimwe haki hiyo, sheria
haitutambui.”<<< Li Tingting.
Watu wameigeuzia macho hii ishu, China
na maamuzi yao ni ishu nyingine ikitokea umevunja Sheria, kuna chochote
kitatokea kwa hawa?
0 comments: