Waumini
wa madhehebu tofauti mkoani Tanga wameanza zoezi la kuliombea taifa
katika mchakato wa uchaguzi mkuu ujao ili uweze kufanyika kwa amani na
utulivu pamoja na kupata viongozi ambao watajali maslahi ya watanzania.
Wakizungumza
katika ibada maalum ya kuliombea taifa pamoja na kuwasimika baadhi ya
viongozi wa makanisa mbalimbali wamewataka watanzania kuacha kushabikia
vyama na badala yake wachague viongozi ambao wataendelea kudumisha
utaifa na kusimamia sera ambazo zitaleta maendeleo kwa taifa.
Aidha askofu wa kanisa la Free Pentekoste jimbo la Tanga mchungaji John Mwakyusa amewataka viongozi wa itikadi za vyama tofauti kutumia vyema majukwaa ya kisiasa katika kampeni zao kutoa lugha ambazo zitakuwa na elimu ndani yake kwa wananchi
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya viongozi wakuu wa madhehebu nchini wamewataka baadhi ya viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu kusimamia na kutekeleza ahadi zao ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ambayo imesababisha maafa katika maeneo tofauti hapa nchini.

0 comments: