Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI,George Simbachawane amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga ‘debe’ wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu.
Amesema kazi ya kupiga debe sio rasmi na haina kipato kinachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini.
Namuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uhalifu katika maeneo ya vituo vya mabasi hivyo wanapaswa kuondolewa haraka wakafanye shughuli nyingine kama kilimo.
Hivi karibuni akiwaapisha wakuu wapya wa mikoa, Rais Dkt. John Magufuli aliwaagiza kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (pool table) nyakati za asubuhi na kuwataka wajiingize kwenye shughuli maendeleo kama kilimo.
0 comments: