Mchekeshaji Athuman Ford ‘Wabogojo’ amesema Mr. Nice ndiye
aliyemtoa na kumfanya ajulikane kwa watu, hivyo kwake ni sawa na bosi
wake na kila akirudi hapa nchini lazima aende nyumbani kwake kumjulia
hali.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Wabogojo amesema kupata shavu katika video ya wimbo Kikulacho wa mkali wa Tekeu, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ miaka ya 2000, kumempa mafanikio makubwa sana.
“Mr. Nice ndio bosi wangu, Mr. Nice ndio ambaye alifanya Watanzania, Wakenya, Wauganda na mataifa mbali mbali wakanitambua mimi, Mwenyezi Mungu alimtumia Mr. Nice kuninyanyua mimi, hata kama labda sijapata pesa nyingi sana kipindi niko na Mr. Nice lakini kitu nilichokipata kutoka kwa Mr. Nice ni zaidi ya fedha hata mi mwenyewe namwambiaga, ndio maana mpaka sasa hivi yule jamaa namuheshimu, kila nikirudi lazima niwasiliane nae na naendaga mpaka kwao”, alisema Wabogojo ambaye pia ni kaka wa msanii wa bongo movies Shamsa Ford.
Pamoja na hayo akielezea changamoto ya kufanya sanaa nje ya nchi yake, Wabogojo amesema alikuwa anapata shida siku za mwanzoni kutokana na lugha ya Kiswahili aliyokuwa akitumia, kushindwa kuwasiliana na watu wa jamii ya huko.
“Changamoto kubwa ilikuwa, lugha sisi ni waswahili hata shule hatutumii english, unaenda supermarket kununua lotion unanunua sabuni, tulikuwa tunajifunza pia kuishi mazingiraya kule”, alisema Wabogojo.

0 comments: