Hata hivyo jaji anayeendesha kesi hiyo, Ann Nevins aliamua kumbana 50 kutokana na tabia yake ya kuonesha fedha kwenye Instagram ilhali anasema amefilisika.
Wakili wa rapper huyo alidai kuwa fedha hizo ni feki. Pia 50 Cent aliikana kauli yake ya awali kuwa anamiliki mjengo wa kifahari Afrika.
Na sasa TMZ imepata sauti kutoka mahakamani ambayo anasikika mwanasheria wa 50 akimueleza jaji kuwa mteja wake ni lazima aonekane ana fedha ili kuwafurahisha mashabiki wake huku pia akiilinda brand yake.My crib is almost finished in AFRICA. I'm gonna have the craziest House warming party ever. I'll… https://t.co/eZXiYL8jpn— 50cent (@50cent) September 5, 2015
Kwenye sauti hiyo wakili anasikika akisema:
Sitakuomba iwapo usikilize muziki wake au kama umeshaona video zake au kitu chochote kama hicho, lakini ukimuangalia Bwana Jackson au wasanii wengine wa Hip Hop, wana ushawishi. Wanatoka kwenye umaskini. Mashabiki wao wengi ni maskini. Wanataka rapa wanayempenda awe tajiri. Fedha ni muhimu kwao. Angalia baadhi ya video zake, fedha ni muhimu. Kutangaza kufilisika kwa tafsiri iliyotolewa ni changamoto kubwa ya jinsi inavyoenda kushughulikiwa.
Pia wanasheria wake wanadai kuwa kama 50 akiishi ya kweli ni ngumu kupata deal za matangazo, TV au movie.
0 comments: