Monday, 14 March 2016

Kayumba: Sikujua kama Fella na Tale watamsimamia mshindi wa BSS

From zero to hero. Kwa sasa huo ndio msemo ambao Kayumba atakuwa anautaja kila siku.

Baada ya kuachia wimbo ‘Katoto’ na kuzidi kufanya vizuri kwenye media na video yake kuwa na ubora, mshindi wa BSS season 5, Kayumba Juma amesema hakujua kama Fella na Tale watakuwa wasimamizi wakuu wa mshindi wa BSS.
Akiongea na Bongo Kali inayoruka kupitia City fm Radio, alhamisi iliyopita, Kayumba alisema, “Mwanzo kabisa wakati mashindano yakiendelea sikuwa najua kabisa kama mshindi wa BSS atakuwa chini ya Fella na Tale. Kiukweli nilishtuka sana siku ambayo tulitangaziwa kuwa hao ndio watamsimamia mshindi, niliona kuwa hapo ndio nyumbani tena.”
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: