Home
News
WALIMU WANAOTUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAUNDIWA KAMATI
WALIMU WANAOTUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAUNDIWA KAMATI
in
News
published on 21:56:00
Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mwanza kimeunda kamati kuchunguza
tuhuma dhidi ya baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Mihama wilayani
Ilemala kujamiiana na wanafunzi wao.
Mwenyekiti wa CWT mkoani hapa, Sibora
Kisheri alisema wameunda kamati hiyo baada walimu wanane, akiwamo mkuu,
Joseph Marifedha kusimamishwa kazi kwa amri ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa
huo, Magessa Mulongo kwa tuhuma hizo.
“Haiingii
akilini kuona walimu wote wakawa na sifa ya makosa yanayofanana, hivi
hakuwapo hata mmoja aliyeshtukia mchezo huo na kuwashauri wezake,” alisema Kisheri.
Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini
kiini cha tuhuma hizo na kuishauri Serikali na vyombo husika hatua
stahiki za kuchukua kuhakikisha kila upande unatendewa haki.
Aliwaasa walimu kufuata sheria, kanuni na misingi ya kazi kwa kutimiza wajibu na kuepuka mambo yanayokinzana na taaluma hiyo.
Hivi karibuni Mulongo aliwasimamisha walimu hao baada ya kupata taarifa kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.
0 comments: